Best posts made by robot
posted in General Discussion read more

Taarifa ambazo tumezipata muda huu Mwanasheria Mkuu wa Chadema Tundu Lissu anatarajia kupelekwa mahakama ya Kisutu muda huu. Baada ya kukamatwa jana kwa tuhuma ambazo haziwekwa wazi.

https://www.jamiiforums.com/threads/tundu-lissu-kupandishwa-mahakama-ya-kisutu-muda-huu.1218181/

posted in General Discussion read more
nasmapesa

nasmapesa JF-Expert Member


Salaam zikufikie popote ulipo.

Niende moja kwa moja kwenye point,kupitia wizara yako ulitoa waraka kwa watumishi kuhamishwa(ikama) kwa walimu katika kila halmashauri na ukasisitiza mambo haya yafanyike haraka na kwa ufanisi.

Cha kusikitisha mpka leo hii kuna baadhi ya walimu hawakupewa hata senti ya uhamisho ambayo kwa mujibu wa sheria ni lazima watu hawa walipwe mana ni stahiki zao hii inauma sana,unamtoa mtu mjini wala hakuomba unampeleka kijijini kwa kumuahidi utamlipa then unaacha kumlipa kwa wakati bila sababu za msingi.

Lakini pia baadhi ya halmashauri zimeenda mbali zaidi kwa kufanya zoezi hili kama kukomoana mfano halmashauri ya wilaya ya Korogwe kilichofanyika mh waziri ni dharau sana nenda kashuhudie.

Huko jiji la Tanga nako walimu wanalia ukienda Tabora hali ni hiyo hiyo.

Nikuulize waziri, ulikuwa na sababu gani kutoa waraka kama hukujipanga kifedha? Kwanini usitafute fedha kwanza? Kama ulitoa hizo fedha ulizifuatilia lini kujua matumizi yake Kama ni sahihi?

Tunakuomba aidha wewe au naibu waziri mrudi mkoa wa Tanga muone matatizo waliyonayo watumishi wa umma.

Mkurugenzi wa jiji la Tanga anajitahidi sana ila kuna watu wanamkwamisha sana,wakiongozwa na maafisa utumishi.

Nakala :N/w wizara tamisemi
:Wadau serikali kuu

https://www.jamiiforums.com/threads/waziri-wa-tamisemi-shughulikia-masuala-ya-uhamisho-kwa-watumishi-wa-umma.1208459/